Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia, (akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani),ameitaka
serikali kuchukua hatua kuhakikishi milio ya kupokelea simu yenye
maudhui ya kidini pale unapompigia mtu simu isitishwe nara moja...Mh.Mbatia ameyasema hayo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani.
Mh.Mbatia
ametoa mfano kwamba hata sasa unaweza kumpigia simu afisa wa ngazi ya
juu wa jeshi la polisi na utakuta simu yake inatoa mlio wenye maneno au
ujumbe wa dini yake.
Mh.Mbatia
alitoa mfano wa maneno kama "pepo toka" maneno ambayo mtu huyasikia
pale unapompigia mtu simu na kudai kuwa yanachochea vurugu za
kidini na kuleta mgawanyiko miongoni mwa watanzania
|
No comments:
Post a Comment