Ilikuwa
mwezi wa 10 mwaka 2005 nilipojiunga na chuo kikuu cha Dar es Salaam
kusoma shahada yangu ya kwanza ya Sayansi katika Uhandisi wa Kompyuta na
Teknolojia ya Habari (Bsc. in Computer Engineering and IT). Mimi pamoja
na vijana wenzangu tuliotoka kwenye familia zilizo na uwezo wa kawaida
sana na ambao ki msingi ni familia za wakulima za huko vijijini hapa
nchini tulikuwa na wakati mgumu kidogo kuendana na mazingira ya chuo
kikuu na jiji la Dar es Salaam kwa ujumla. Wanafunzi wa kiume
waliochaguliwa kusoma shahada hii wengi wetu tulipewa vyumba vya malazi
(accommodation) katika ghorofa moja pale kampasi kuu (main campus) jengo
namba 2 (hall 2) ghorofa ya 7 na 8 (7th and 8th floor). Baada ya
kujiunga na chuo tulitegemea kuanza kupatiwa sehemu ya mkopo kwa
wanafunzi kwaajili ya chakula, malazi na vifaa vya kusomea (meal,
accommodation and stationary) wakati huo ikiwa ni asilimia mia (100%).
Badala yake mkopo huo ulichelewa kwa zaidi ya wiki mbili na kusababisha
adha kubwa kwa wanafunzi pale chuoni. Ilitulazimu kuanza kuwasiliana na
ndugu jamaa na marafiki ili kupata walau vijisenti vya kujikimu. Bahati
mbaya mkopo uliendelea kuchelewa hadi kufukia kiasi wanafunzi kuanzisha
mgomo mkubwa ukiongozwa na Raisi wa serikali ya wanafunzi (DARUSO) na
waziri mkuu wake, wakati huo Mwita Waitara na John Mrema.
Sikuchache kabla ya mgomo huo sisi tulianzisha mtindo maarufu wa
KUPUNGUZA KULA KUBANA MATUMIZI uliokuwa ukiitwa "KUPIGA DESH ama PASI
NDEFU", siku moja nilijikuta nikipiga pasi ndefu sana hadi nikadhoofika,
nikaacha vipindi darasani na kwenda chumbani HALL II kulala, kwa bahati
mbaya ama nzuri mwenye funguo wa chumba hakuacha funguo mahali ambapo
huwa tunaweka, ikanilazimu kwenda kulala chumba cha jirani kwa rafiki
yangu Musa Chibali Semwenda niliyekuwa nikisoma naye darasa moja pamoja na Edgar Tenga, Beatus FK, Linda Joseph, Irene Dubi Makundi, Paul G Mandu, William Nzunda, Hellen Maziku, Irene Kemilembe Joseph,
.... Kilichotokea baada ya kulala sikupata fahamu tena. Baadae nimekuja
kuzinduka Musa Chibali Semwenda ananinywesha chai na mkate. KUMBE
NILIZIMIA KWA NJAA!. Baada ya kupata chakula kile nilipata nguvu kidogo
na kisha kwenda zahanati ya chuo na daktari akaniambia ulikuwa umekaa
muda mrefu sana bila kula. Mgomo ulipoanza nilishiriki kikamilifu huku
nikiwa na maumivu makubwa moyoni kwamba ningekufa kwa njaa mie kama sio
kusaidiwa na rafiki mwema. POLICE WANGENIPIGA NA KUNIUA KWA RISASI AMA
MABOMU LAKINI NILIKUWA NAJUA NINACHOTETEA. "SINTOACHA KUPAMBANA KUTETEA WANYONGE WENZANGU HADI PUMZI YANGU YA MWISHO"
Hizi ni salamu kwa Waziri Mkuu Mizengo Kayanza Peter Pinda (Mtoto wa
Mkulima aliyesahau Wakulima wenzie kwa ulevi wa Madaraka) kauli yako ya
juzi imezidi kunitia maumivu, na kunikumbusha yale mabomu tuliyopigwa na
police miaka 8 iliyopita.
|
No comments:
Post a Comment