LIWALE: WATOTO WADOGO WABAMBIKIZIWA KESI YA "UNYANG'ANYI" WA KUTUMIA SILAHA.
Watoto SAID HASSAN BADI, 14 (Kushoto kwangu) na SALAMA HASHIM MBWANA,
14 (Kulia kwangu) - (wote wanafunzi wa kidato cha kwanza) wakiwa
mahakama ya wilaya ya LIWALE mara baada ya kusomewa mashtaka kwenye kesi
zaidi ya tatu. Katika kesi moja watoto hawa wanatuhumiwa kuvamia duka,
kulivunja, kuona na kumtishia mwenye duka (mwanaume) watamuua kwa
silaha. Nilipoongea na watoto hawa nilishangaa sana, huyo wa
kiume anasema siku ya matukio ya wananchi kufanya vurugu yeye alikuwa
anaangalia mpira, aliposikia milio ya risasi majira ya jioni alikimbia
kutoka ukumbini, njiani akakutana na mjomba wake ambaye ni diwani wa
CCM, mjomba wake akamuuliza anakimbia nini? Akamjibu kuwa ameambiwa kuwa
kuna vurugu hivyo anakimbilia nyumbani. Diwani wa CCM akamwambia
anawajua vijana waliomjulisha kuhusu vurugu? Kijana huyu akajibu
hawajui, ndipo mjomba mtu(diwani) akaanza kumpiga makofi, na mwisho wa siku kijana huyu akakimbilia kwao.
Keshoye akaamkia shuleni, akiwa shuleni mjomba wake akaja na polisi,
wakamkamata. Hajui lolote kuhusu matukio hayo lakini anasomewa shtaka la
kuona kwa kutumia silaha usiku wa manane. Huyu
SALMA(msichana), anasema siku moja baada ya matukio ya LIWALE, polisi
walifika nyumbani kwao(Yeye Salma na mama yake wanasimamia nyumba ya
ndugu yao yenye wapangaji). Polisi walipofika wakamkamata mpangaji mmoja
na kusachi chumba cha mpangaji huyo. Baadaye polisi wakaondoka na
mpangaji huyo pamoja na DRYER ya Saloon na kiti cha
Saloon(vinavyosemekana kuwa vya wizi). Baada ya muda kidogo,
polisi wakarudi na wakaanza kumpiga sana msichana huyu na mama yake,
wakawakamata na kuwaweka Rumande. Yule mpangaji alokutwa na vitu vya
wizi aliachiwa kesho yake na hajapandishwa kizimbani. Hadi mtoto huyu na mama yake wanafikishwa mahakamani hawakuwahi kujua kosa lao ni nini.
Wamefikishwa mahakamani na kushtakiwa kwa kesi 4 tofauti. Katika kesi
mojawapo, mtoto huyu anatuhumiwa kwa kesi ya unyang'anyi wa kutumia
silaha na haina dhamana.
|
No comments:
Post a Comment