Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha
shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea asubuhi hii saa 5:16 (11:16 am) inavyosemekana mdada huyo
alikua akitoka benki ya CRDB tawi la
Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo.aliposimama
ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na
kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.Bado hazijapatikana taarifa zaidi za kujua mama huyo ni nani na anaishi maeneo yapi hapa jijini Dar. Pia bado hakuna taarifa za kukamatwa wahusika wa tukio hilo.
|
No comments:
Post a Comment