Friday, May 10, 2013

MLIPUKO WA BOMU ARUSHA: MAJERUHI AELEZA BOMU LILIVYOKUWA

Majeruhi wa mlipuko wa bomu Arusha, Mwalimu Fatuma Tarimo akionyesha kipande cha chuma  baada ya kuondolewa kwenye mguu wake, katika Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam jana.
Kwa ufupi
“Baada ya kutua, nilisikia kishindo kikubwa nikashtuka ikabidi niangalie. Baada ya kuona ni kitu kama chuma nilipata hofu nikafikiria kuondoka,”
HABARI ZAIDI
BOMU lililorushwa na kuua watu watatu na kujeruhi wengine zaidi ya 60 kwenye Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi huko Arusha, inadaiwa lilitengenezwa kienyeji.
Wakati kukiwa na madai hayo, mazishi ya marehemu hao Regina Kurusei, (45), James Gabriel (16) na Patricia Joachim (9) yanatazamiwa kufanyika leo Olasiti, Arusha na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda anatarajiwa kuhudhuria.
Ofisa mstaafu wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini, alimdokeza mwandishi wetu jana kuwa kwa ujuzi na uzoefu wake wa masuala hayo, bomu hilo si la kiwandani akisema msingi wa imani yake ni jinsi vyuma vilivyotawanyika na kuumiza watu zaidi ya 20.
Watu saba wamefikishwa kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa ajili ya kuondolewa vyuma na kupata matibabu zaidi.
Mstaafu huyo alieleza kuwa mabomu mengi zaidi ya kienyeji hutengenezwa kwa kutu
mia bakuli za chuma, zikiwekewa baruti ndani na kufungwa kwa waya.
“Hawa jamaa huweka vipande kama 36 vya baruti na hufungiwa ndani ya bakuli kwa kubanwa sana ili kuvipa joto na bomu likitua, husababisha madhara makubwa,” alisema ofisa huyo ambaye alishiriki Vita ya Uganda mwaka 1978 hadi 1979.
Mstaafu huyo alisema mabomu ya aina hiyo yametumika kwenye mashambulizi ya kigaidi katika nchi mbalimbali duniani kama Lebanon, Vietnam, Libya, Ireland Kaskazini, Syria, Afghanistan, Iraq, Chechnya na India.
Mmoja wa majeruhi, Mwalimu Fatuma Tarimo amesimulia alivyoshuhudia bomu likitua mbele yake na kulipuka.
Tarimo, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, alisema jana kuwa aliliona bomu hilo likiwa na rangi ya shaba. Pia alisema lilikuwa na waya kwa juu.
“Baada ya kutua, nilisikia kishindo kikubwa nikashtuka ikabidi niangalie. Baada ya kuona ni kitu kama chuma nilipata hofu nikafikiria kuondoka,” alisema mwalimu huyo wa Shule ya Msingi ya Burka Estate, nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Hata hivyo, alisema kabla ya kuondoka, alishtukia amenyanyuliwa juu na hakujua kilichoendelea kwani aliposhtuka alijikuta akiwa katika Hospitali ya Mount Meru.
Tarimo ametolewa kipande cha chuma katika mguu wake wa kulia.
“Nina maumivu bado lakini nina matumaini nimechukuliwa kipimo cha ‘T-Scan’ kwa matibabu zaidi,” alisema Mwalimu Tarimo ambaye anaaminika kuwa na kipande kingine kwenye mapafu.
Majeruhi mwingine, Jenipher Joackim ambaye amefiwa na mwanaye Patricia Joackim (9) hana taarifa za kifo hicho kilichotokea katika Hospitali ya KCMC.
“Nimeambiwa kwamba yupo ICU sijui anaendeleaje,” alisema.
SOURCE: Mwananchi

Wednesday, May 8, 2013

LWAKATARE AFUTIWA MASHTAKA YA UGAIDI

Mahakama Kuu ya Tanzania imefuta mashtaka yote ya ugaidi yaliyokuwa yanamkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa CHADEMA Wilfed Lwakatare.

Taarifa kutoka Mahakama Kuu zinasema Mahakama Kuu imebakiza shitaka moja tu, la utekaji ambalo kimsingi ni Jinai na lina dhamana.

MBATIA: MIITO YA SIMU YENYE MILIO YENYE MAUDHUI YA KIDINI ITOLEWE!

Mbunge wa kuteuliwa Mh. James Mbatia, (akichangia bajeti ya Wizara ya Mambo ya Ndani),ameitaka serikali kuchukua hatua kuhakikishi milio ya kupokelea simu yenye maudhui ya kidini pale unapompigia mtu simu isitishwe nara moja...Mh.Mbatia ameyasema hayo leo bungeni wakati akichangia bajeti ya wizara ya mambo ya ndani.
Mh.Mbatia ametoa mfano kwamba hata sasa unaweza kumpigia simu afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la polisi na utakuta simu yake inatoa mlio wenye maneno au ujumbe wa dini yake.

Mh.Mbatia alitoa mfano wa maneno kama "pepo toka" maneno ambayo mtu huyasikia pale unapompigia mtu simu  na  kudai  kuwa  yanachochea  vurugu  za  kidini  na  kuleta  mgawanyiko  miongoni  mwa  watanzania 


Monday, May 6, 2013

MWANAMKE AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI KIFUANI NA WATU WANAOSADIKIWA KUWA NI MAJAMBAZI KARIAKOO DAR

Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea asubuhi hii saa 5:16 (11:16 am) inavyosemekana mdada huyo  alikua akitoka benki ya CRDB tawi la
Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikuwa yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo.
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.Bado hazijapatikana taarifa zaidi za kujua mama huyo ni nani na anaishi maeneo yapi hapa jijini Dar. Pia bado hakuna taarifa za kukamatwa wahusika wa tukio hilo.

Sunday, May 5, 2013

TUKIO LA MLIPUKO KATIKA KANISA LA MT. JOSEPH OLASITI ARUSHA-TANZANIA






Mlipuko unaodhaniwa kutokana na bomu la kurushwa kwa mkono umetokea katikati ya ibada katika kanisa katoliki la Mt Joseph lililopo Olasiti Jijini Arusha ambako kwa siku ya elo kulikuwa na ibada ya Kuzindua Parokia ya Mt Joseph Olasiti. Mlipuko huo unaelezwa kutokea majira ya katikati ya saa nne na saa tano asubuhi wakati Askofu wa Kanisa hilo akiendelea na ibada. Ibada hiyo sambamba na uzinduzi husika imeahirishwa hadi wakati mwingine.
Balozi wa Papa na ujumbe wake walikuwa miongoni mwa wageni muhimu katika tukio hilo la uzinduzi. Balozi huyo (tutakupatia jina lake baadae) alikuwa Arusha tangia alahamisi ya Mei 2, 2013 na alipatiwa ulinzi wa kutosha na Jeshi la Polisi.
Haijaweza kuthibitika hasa sababu za wahusika kurusha “bomu” lakini mmoja wa washukiwa tayari ametiwa nguvuni na Polisi.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinaeleza kuwa takribani watu wawili wanahisiwa kuwa wamefariki na makumi wengine kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa hopsitali ya Mt Meru kwa matibabu.
Viongozi mbalimbali wa kijamii na kiserikali wameweza kufika eneo la tukio, miongoni mwao akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, Meya wa Manispaa ya Arusha, Gaudence Lyimo, na Mbunge wa Arusha Mjini Mh Gobless Lema.
Wengine ni Mbunge wa Arumeru Mashariki, mh Joshua Nassari, Diwani Msofe wa Kata ya daraja Mbili (CHADEMA), diwani wa Kata ya Olasiti na viongozi wengine wa Jeshi la Polisi na usalama Mkoa na Wilaya.

Jengo la kanisa halijadhurika lakini taharuki miongoni mwa watumiaji wa jengo hilo wakiwemo waumini wa kaisa hilo ni kubwa.

Chanzo  cha  mlipuko  huo  inasemekana   kuwa  kuna  gari  ndogo  ilifika  kanisani  hapo  na  kusimama. Baadae  alishuka  mtu  aliyekuwa  amevalia  vazi  mithili  ya  kanzu  na  kurusha  kitu  kuelekea  kanisani  ambacho  ndicho  kilichosababisha  mlipuko  huo..
Lema hospitaliniMbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akiwa na mbunge wa Arumeru Joshua Nassari wametoa damu kwa ajili ya majeruhi walioumia katika mlipuko huo.

Lema amewahimiza wakazi wa Arusha na vijana kujitolea kwa wingi kuchangia damu ili kuokoa maisha ya majeruhi.  Watu wengi wameitikia wito na  wanaendelea kujitolea kuchangia damu kama ishara ya kumuunga mkono mbunge wao.

Saturday, May 4, 2013

HUU NDIO MKWARA WA WAASI WA "M23 wa DRC" KWA MAJESHI YA TZ na SA!

Kutoka kwenye ukurasa wao wa Twitter!

NASSARI ASEMA YEYE NA LEMA WANAWINDWA WAJERUHIWE

Nikiwa kwenye mazungumzo na mwanausalama mmoja wa Hapa Arusha, amenijulisha kuwa Wanausalama wa Arusha wameazimia kutujeruhi mimi na Mhe. Lema kwa sababu ya harakati zetu mkoani Arusha lengo likiwa ni kurudisha nyuma morali na kuwaingizia hofu wananchi. Nanukuu kilichosemwa, "sasa tutawavunjavunja kabisa miguu hawa wawili, ngoja tu" mwisho.

SOURCE:  Josh Nassari, facebook account.

Friday, May 3, 2013

MSIGWA AMSHANGAA WAZIRI WA J.K

 Haya ndio maneno ya Mh. Msigwa just now via Facebook:
"Waziri wa JK hajui tofauti kati ya wetlands na game controlled area.....mambo ya ajabu kabisa haya. Waziri huyu anasema game controlled area ni eneo Oevu,,,,,shame on this gorverment ."

MFANYA BIASHARA KARIAKOO AJIRUSHA TOKA GOROFA YA TISA NA KUANGUKIA GARI


Muda mfupi uliopita,Mtu mmoja alietambulika kwa jina la Shirima ambaye ni Mfanyabiashara katika moja ya Maduka ya Kariakoo jijini Dar es Salaam,amejirusha toka ghorofa ya 9 ya Hoteli ya Concord iliopo Maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam na amekimbizwa hospitali kwa uangalizi zaidi maana haijafahamika kama kapoteza Maisha au bado yu hai.

Mfanyabiashara huyo alijirusha toka ghorofani na kuangkia katika Gari aina ya Toyota Corolla ambayo ni taxi iliyokuwa imepaki nje ya hoteli hiyo,chanzo cha kujirusha kwa mfanyabiashara huyo bado hakijafahamika mpaka sasa.

Mashuhuda wa tukio hilo lililotokea muda mfupi uliopita,wanaeleza kuwa walipatwa na mshtuko baada ya kusikika kishindo cha kitu kilichokuwa kimeangukia gari hilo na waliposogea kushuhudia ndipo walipobaini kuwa alikuwa ni mtu huyo alietambulika kwa jina moja la Shirima.